Askari Polisi kikosi kazi cha taifa cha kupambana na ujangili, E.1180 Koplo Emmanuel ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jinsi alivyomuhoji kwa zaidi ya saa mbili raia wa China, Yang Feng Glan ‘Malkia wa Tembo’.
Mbali ya Glan, washtakiwa wengine ni Salvius Matembo na Philemon Manase ambao kwa pamoja, wana kesi ya kufanya biashara ya vipande 706 vya Meno ya Tembo yenye thamani ya Sh.Bilioni 13 ambapo walitenda kosa hilo January Mosi, 2000 na May 22,2014.
Mahojiano hayo yalifanyika September 28, 2015 asubuhi ambapo baada ya mtuhumiwa Glan kuelezwa haki yake ya kufanyiwa mahojiano akiwepo mtu yeyote wa karibu anayemuhitaji aliomba awepo jamaa yake aitwaye Manfred Lyoto.
Baada ya kutoa ushahidi huo, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi. aliahirisha kesi hiyo hadi November 30, 3017 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.
Ulipitwa na hii? Shahidi kesi ya Malkia meno ya Tembo hajatokea Mahakamani
MENGINE YALIYOIBUKA KIFO CHA ALIYEMKAMATA MALKIA MENO YA TEMBO