Kila anaefatilia siasa anajua Benard Membe ni miongoni mwa Wanasiasa maarufu ambao hawajaonekana tena kwenye majukwaa wakiongea baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Wiki hii Waziri huyu wa zamani wa mambo ya nje na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Mtama alitokea kwenye kufungua Msikiti wa Masjid IDHIHAL kijiji cha Kiwalala ambapo ameahidi kusaidiana na Mbunge wa sasa wa Nape Nnauye kuumalizia Msikiti huo.
Aliposhika kipaza sauti Membe alizungumza yafuatayo >>> “Kiwalala ndipo panapozaa Mbunge, ukishindwa kupata kura hapa huwezi kuwa Mbunge, nilianzia kupata kura hapa nikawa Mbunge wa miaka 15 ndio maana hata ingetakiwa Misikiti 6 tutaijenga tu“
“Na Mufti ningependa ujue kwamba katika Jimbo letu la Mtama Asilimia 62 za Wakazi wote ni Waislamu na Asilimia 38 ni Wakristo, mimi nilikua nachaguliwa na Waislamu hata kama Wapinzani wangu niliokua nasimama nao walikua Waislamu, nikajua huu ni mtego wa Mwenyezi Mungu lazima nilipe”
MTAZAME ZAIDI BENARD MEMBE AKIONGEA KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI…
NAPE: “WATU WANAKATANA MAPANGA, SISI WANASIASA TUNAWEZA KUSHINDWA KUHIMILI”