Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetupilia mbali maombi ya upande wa utetezi katika kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali za Bil.3.6 kinyume na mshahara inayomkabili Mhasibu wa zamani wa (Takukuru), Godfrey Gugai.
Maombi ya upande wa utetezi yalilenga kuiomba mahakama hiyo kuyaondoa mashtaka 23 ya utakatishaji fedha yanayomkabili Gugai na wenzake.
Uamuzi wa kuyatupa maombi hayo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa serikali, Peter Vitalis kusema shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya uamuzi.
Kabla ya kuahirisha kesi hiyo hadi December 28, 2017, Hakimu Simba alisema mahakama hiyo inatupilia mbali maombi ya utetezi kwa madai mashtaka 23 ya utakatishaji fedha yapo kimakosa katika hati ya mashtaka.
“Hati ya mashtaka ipo sahihi, hivyo natupilia mbali maombi hayo na upande wa Jamhuri unaweza kuendelea na hatua za upelelezi.” – Hakimu Simba.
Ulipitwa na hii? Waliosababishia hasara ya Sh.milioni 370 kwa TCRA wafikishwa Mahakamani