Upande wa mashtaka katika kesi inayowakabili vigogo wa kampuni ya mawasiliano ya Six Telecoms, akiwemo Wakili maarufu Dk.Ringo Tenga na mfanyabiashara Peter Noni, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa utajitahidi kukamilisha upelelezi.
Mbali na Dk. Tenga na Noni, washitakiwa wengine ni Mhandisi na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Hafidhi Shamte, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo, Noel Odeny Chacha na Kampuni ya Six Telecoms Limited.
Hayo yameelezwa na Wakili wa Serikali, Jacquline Nyantori mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa wakati kesi hiyo ilipotajwa akidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, hivyo anaomba kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine kwa kutajwa.
Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Nongwa alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kufanya lolote katika kesi hiyo hadi upelelezi utakapokamilika ama kitakapotolewa kibali na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuruhusu kesi hiyo isikilizwe hapo na kuiahirisha kesi hiyo hadi December 12, 2017.
Ulipitwa na hii? Waliosababishia hasara ya Sh.milioni 370 kwa TCRA wafikishwa Mahakamani