President John Pombe Magufuli leo December 10 2017 amekutana na Viongozi wa Jeshi la Magereza kwenye Ikulu ya Chamwino Dodoma ikiwa ni siku moja toka atoe msamaha kwa Wafungwa mbalimbali kwenye sherehe za miaka 56 ya Uhuru.
Rais Magufuli ametia saini nyaraka za msamaha alioutoa jana kwa Wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa na wawili Wanamuziki maarufu Papii Kocha na Babu Seya waliohukumiwa kifungo cha maisha gerezani.
Namnukuu alichowaambia Viongozi hao wa Magereza >>> “Nimeona nitumie kifungu hiki cha Katiba ambacho hakijawahi kutumika, unajua mtu ambae alihukumiwa kunyongwa alafu baadae anaachiwa ni kitu cha kushangaza hakijawahi kutokea”
“Hakijawahi kutokea lakini nimeona nifanye hivyo kwa ajili ya Watanzania, niwaombe muendelee kusimamia wajibu na sheria, Mtu anaehukumiwa kufungwa afungwe kweli na nilishatoa wito kwa Magereza pasiwepo Wafungwa wa kukaa tu na kupumzika, wafanye kazi kufungwa sio kustarehe”
Kwenye hatua nyingine President amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kutekeleza agizo lake la kutengeneza viatu kwa ajili ya Askari wake badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi.
Baada ya maneno hayo ya JPM, Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa ambae amemshukuru Rais Magufuli kwa kutoa msamaha huo wa kihistoria na kusema Wafungwa wote waliopewa msamaha huo wameachiwa huru kutoka kwenye magereza toka jana.
Jeshi la Magereza linazalisha jozi 150 za viatu kwa siku katika kiwanda chake cha Karanga kilichopo Moshi Kilimanjaro ambapo kwa kushirikiana na mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF limeanza kuboresha kiwanda hicho ili kufikia uzalishaji wa jozi 450 kwa siku.
HD VIDEO: RAIS MAGUFULI ALIVYOTANGAZA KUWASAMEHE BABU SEYA NA PAPI KOCHA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA
BABU SEYA NA PAPI KOCHA WALIVYOMFATA MCHUNGAJI BAADA YA KUTOKA TU GEREZANI