Serikali ya Tanzania imepata mkopo wa Tsh.Bilioni 630.25 kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Tabora.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amewaambiwa waandishi wa habari kuwa katika fedha hizo za mkopo serikali ya Tanzania itachangia Tsh.Bilioni 72 kwa ajili ya ujenzi huo.
Prof. Mbarawa amesema kuwa mradi huo utahusisha barabara za Tabora (Usesula)-Koga-Mpanda yenye urefu wa Kilometa 335.979 na Mbinga-Mbamba Bay yenye Kilometa 67.
Prof. Mbarawa alisema sehemu ya kwanza ni Usesula hadi Komanga ikihusisha barabara unganishi za mji wa Sikonge wakati sehemu ya pili ni Komanga hadi Kasinde ikihusisha barabara za mji wa Inyonga na ya tatu Kasinde hadi Mpanda ikihusisha barabara za mji wa Urwirwa.
Ulipitwa na hii? Kamishna wa Magereza TZ afunguka kuhusu msamaha wa JPM jana