Kundi la kigaidi la Al-Shabab ambalo limekuwa likitekeleza mauaji maeneo mbalimbali ndani ya Taifa la Kenya na maeneo jirani kundi hilo limetoa tishio la kufanya mashambulizi katika Mji wa Lamu nchini humo.
Kamishina wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lamu, Gilbert Kitiyo amesema kuwa wapiganaji hao kutoka Jaysh Ayman ambacho ni kikundi cha Kiislamu kinachohusishwa na Al-Shabaab kinaweza kuwa kinapanga mashambulizi wakati wa msimu huu wa sikukuu.
“Vuguvugu la Jaysh Ayman limeonekana upande wa Ijara. Hatuwezi kuketi na kusubiri wapigananji hao kufanya mashambulizi na kuwauwa watu tena. Tunawaomba Raia kutoa ripoti kwa Polisi itakayosaidia kushambulia kambi yao.” -Kitiyo
Kulingana na ripoti ya Standard Digital, wapiganaji hao ni pamoja na Wakenya na raia wengine wakigeni ambao wamehusika siku za hapo awali kufanya mashambulizi katika maeneo ya Lamu, Tana River na Garissa tangu mwaka 2014.
Kamishna Kitiyo amesema kuwa wapiganaji hao walikuwa wameonya kutekeleza mashambulizi katika sherehe za Jamhuri, sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya
Haya yanajiri baada ya wakazi kutoroka kambi za wakimbizi kutokana na mashambulizi kadhaa yaliyosababisha vifo vya maafisa watatu wa polisi eneo la Pandanguo na wanaume tisa katika kijiji cha Jima.
BABU SEYA NA PAPI KOCHA “WAMETUNGA NYIMBO NYINGI SANA GEREZANI,” BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA