December 14, 2017 Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dr Mwigulu Nchemba amefika katika kijiji Hurui kilichopo Wilaya ya Kondoa ambapo kumekuwa na mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka zaidi ya tisa ambao umekuwa ukihatarisha amani ya Kijiji hicho.
Waziri Mwigulu amewataka Wananchi kuacha kuuza maeneo kinyemela ambayo yanahusisha watu wengi, na kuagiza kutumika kwa mikutano ya vijiji pale ardhi ya Kijiji inapotaka kuuza.
“Acheni kuuza maeneo kinyemela yanayohusisha watu wengi mizozo mingi kwenye vijiji inatokana na kuuza maeneo kinyemela, watu wanakaa kinyemela wawili wakiona sherehe zinakuja, wakiangalia hawana hela wanauza HAKI za watu, acheni kufanya biashara hizo za kinyemela zinazohusisha watu wengi.” – Waziri Mwigulu Nchemba
“Hii si serikali ya ujanjaujanja, si serikali ya dili dili, kwa maslahi ya usalama naelekeza matumizi ya eneo lile yaende kama yalivyo na mtu yoyote atayepinga na kusababisha ukosefu wa usalama tutamchukulia kama mtu anayesababisha uvunjifu wa amani katika eneo hili.” – Waziri Mwigulu Nchemba
“WANASEMA VYUMA VIMEBANA, WEKA GRISI” -JPM, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA