Leo December 15, 2017 Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza mfumo mpya wa ulipaji wa Bill nchini kwa kutumia Government Electronic Payment Gateway (GEPG) ambao umeanza rasmi siku ya jana.
Akiongea na waandishi wa habari, Meneja TEHAMA wa TANESCO Evaristo Winyasi amesema “mfumo huu mpya umeanza rasmi siku ya jana katika mkoa DSM na Pwani, lengo likiwa ni kuunganika na mfumo huu wa serikali ni matakwa ya sheria ya Bunge,”
“Wateja wanahudumiwa kwa njia mbalimbali kwa kutumia Benki na Mitandao ya Simu, lengo kuu ni boresha huduma kwa mteja, kuhakikisha mteja anapata huduma haraka na kwa usahihi,” – Winyasi
BREAKING: MBUNGE UPENDO PENEZA (CHADEMA) ANAZUNGUMZA NA WANAHABARI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA