Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wanne wa Kampuni ya Mawasiliano ya Six Telecoms Limited kuhakikisha December 29, 2017 unaeleza hatua ya upelelezi wa kesi hiyo.
Hatua hiyo, inatokana na Wakili wa Serikali, Jehovaness Zacharia kumueleza Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Kutokana na kauli hiyo, Wakili wa utetezi, Alex Mgongolwa alidai haridhishwi na maelezo ya kutokamilika upelelezi ambapo akautaka upande wa mashtaka kueleza wamefikia katika hatua ipi.
Kutokana na mvutano wa kisheria, Hakimu Nongwa aliutaka upande wa mashtaka kuhakikisha ifikapo December 29, 2017 utoe maelezo ya upelelezi wa kesi hiyo umefikia wapi.
Katika kesi hiyo, washtakiwa ni Mhandisi na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Six Telecoms, Hafidhi Shamte, Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Mwanasheria na Mhadhiri na Mkurugenzi wa hiyo kampuni, Dk.Ringo Tenga, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo Noel Chacha na Kampuni ya Six Telecoms Limited.
Ilipofikia kesi ya BILIONI 8 inayomkabili Wakili maarufu Dk. Tenga