Ikiwa bado Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu anaendelea na matibabu Nairobi nchini Kenya baada ya kushambuliwa kwa risasi, familia ya Mbunge huyo leo December 15, 2017 imeongea na waandishi wa habari.
Alutha Mughwai ni msemaji wa familia ameita waandishi wa habari moja ya jambo alilolizungumza nikushukuru serikali kupitia Makamu wa Rais kwa kumtembelea Lissu pamoja na suala la gharama za matibabu ambazo bunge halija gharamia zikiwa zimepita siku mia moja.
“Kutoka serikalini ambaye amekwenda kumuangalia ni Makamu wa Rais, kama mlivyomsikia alisema ametumwa na Rais kwenda kumjulia hali, zaidi ya yeye hakuna kiongozi mwingine wa serikali alienda kumjulia hali,” – Mughwai
“Hakuna mtu aliyechukua jukumu la kumtibu Lissu, mawasiliano ya mwisho tuliyoyapata toka Ofisi ya Bunge walitaka tufafanue hizo haki za mbunge kutibiwa, tumefafanua na tuna dai haki 4,” – Mughwai
MFUMO MWINGINE WA KULIPIA BILL TANESCO UMEANZISHWA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA