Baada ya uchaguzi wa UVCCM kumalizika na kumpata Mwenyekiti mpya Kheri James, mmoja wa wanachama wa CCM Reginald Fulgence amekutana na waandishi wa habari Dodoma na kuelezea mazingira yanayodaiwa kuwa ya rushwa yalivyofanyika katika uchaguzi huo.
“Wakati Mwenyekiti anazunguza katika mkutano mkuu wa UVCCM Taifa alikemea rushwa lakini rushwa ilitawala uchaguzi, uchaguzi haukuwa sawa kabisa, ukifuatilia kura zote zilizopigwa utakuta tiki zinafanana, nimuombe Mwenyekiti kama inawezekana uchaguzi UVCCM ufutwe,” – Reginald Fulgence
MWENYEKITI WA UVCCM ALIVYOFIKISHWA MAHAKAMANI DODOMA LEO, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA