Leo December 18, 2017 President John Magufuli amefungua Mkutano Mkuu wa 9 wa Chama cha Mapinduzi ambapo ametoa hotuba ambayo amezungumzia mambo mbalimbali. Millardayo.com inakusogezea kauli 10 kubwa ambazo amezizungumza leo.
"Mapato ya chama kwa Mwaka wa Fedha 2014/15 ilikuwa Tsh Bil 29.35 kati ya fedha hizo Bil 21.95 ilikuwa ni ruzuku na michango ya hiari, 2015/16 ilikuwa takriban Tsh Bilion 73. 19 ambapo ruzuku na michango ya hiari ilikuwa Tsh Bil 56.82." Rais @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) December 18, 2017
"Kwa mwaka 2016/17 mapato yalikuwa takriban Tsh Bil 40.01 ambapo ruzuku na michango ya hiari ilikuwa Tsh Bil 27.56, hii inadhihirisha kuwa uwezo wetu wa kujitegemea ni mdogo ni lazima turekebishe hali hii." – Rais @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) December 18, 2017
"Tulipotafuta taarifa kutoka Wizara ya Ardhi tuligundua kuna viwanja vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi zaidi ya 5000 katika nchi hii lakini kwa muda mrefu rasilimali hizi hazijanufaisha wanachama na chama chetu kwa ujumla." – Rais @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) December 18, 2017
"Watu wachache waliojaribu kutishia muungano na umoja wetu tumewadhibiti kikamilifu." – Rais @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) December 18, 2017
"Nilisema kwenye mkutano mkuu uliopita kuwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi hawapaswi kuwaogopa watendaji wa serikali hususani katika kutetea maslahi ya wanyonge." – Rais @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) December 18, 2017
"Nchi yetu ni miongoni mwa nchi chache Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi, aidha mfumuko wa bei unaendelea kushuka, ambapo mwaka huu, hadi kufikia November ulishuka hadi 4.4%." – Rais @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) December 18, 2017
"Vilevile akiba ya fedha za kigen imefika Dola za Kimarekani Mil 5820.4 kwa mwezi October 2017, kiasi hii kinaiwezesha nchi yetu kulipia gharama za kununua bidhaa kwa miezi 5." – Rais @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) December 18, 2017
"Hii ina maana ya kwamba leo hii Watanzania tunaweza kukaa bila kufanya kazi yoyote kwa miezi 5 na tukaendelea kupata huduma kama kawaida, lakini hii haimaniishi kwamba watu waache kufanya kazi." – Rais @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) December 18, 2017
"Nina orodha ya wengine wanaotaka kujiunga na CCM wakiwemo wabunge, kwahiyo tutakuwa tunawapokea mmoja mmoja kwa jinsi tutakavyokuwa tunawatathmini ili tusipokee mamluki kwenye chama chetu." – Rais @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) December 18, 2017
"Yupo mmoja ambaye ameomba sana, yeye ni Mbunge na anataka kurudi na Madiwani 8, hiki ni kimbunga, wataisoma namba." – Rais @MagufuliJP
— AyoTV (@ayotv_) December 18, 2017
JPM: “CCM hata wakibaki watatu, potelea mbali”