Leo December 19, 2017 Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi Richard Kayombo amekutana na waandishi wa habari na kueleza kuwa mtu anapoingia au kutoka nje ya nchi akiwa na kiwango cha pesa anatakiwa atoe taarifa kwenye madawati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwenye viwanja vya ndege na mipakani kwa sababu za kiusalama.
Amezungumza jambo hili alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu suala la mtu aliyekukutwa anaingiza nchini Dola za Marekani Mil 1 sawa na Tsh Bil 24 siku za hivi karibuni.
“Hakuna kodi wala gharama yoyote pindi anapotoa taarifa ya pesa anazosafiri nazo, kutoa au kuingiza nchini, madhumuni si kujua pesa imepatikana wapi bali kujua matumizi ya pesa hiyo.” – Richard Kayombo
MIAKA 11 ILIYOPITA: Walichangia ujenzi wa Zahanati lakini haijafunguliwa hadi leo