Leo December 20, 2017 Rais John Magufuli ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Ofisi za Taifa za Takwimu ambapo amewataka Watanzania na taasisi mbalimbali kutumia takwimu sahihi zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS.
President JPM amewashauri Watanzania kujiepusha na takwimu za upotoshaji zinazosambazwa na baadhi ya watu kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii nchini.
Pamoja na wito huo JPM ameitaka NBS pamoja na vyombo vingine husika kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtu yeyote ama taasisi itakayotoa takwimu za upotoshaji.
“Hizi ndio takwimu sahihi, na nyinyi Ofisi ya Taifa ya Takwimu mkiona mtu anapotosha ukweli huu mkamateni mpelekeni mahakamani akajifunze kupata takwimu sahihi.” – Rais Magufuli
“Haya tunayoyafanya wale ambao walikuwa wanapata fedha za bure lazima watapiga kelele kuwa vyuma vimebana, lakini tunabana vya bure ili kuwaletea wananchi maendeleo, na kwa kweli tutabana sana” – Rais Magufuli
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr. Albina Chuwa amesema kwa kutambua umuhimu wa Takwimu katika kupanga, kutekeleza na kusimamia masuala mbalimbali ya maendeleo na ustawi wa jamii ofisi yake imepiga hatua katika ukusanyaji na utoaji wa Takwimu na hivyo kushika nafasi ya pili barani Afrika.
“Sitaki kuongea mengi, tumebana vyuma vilivyolegea” – JPM