Leo December 20, 2017 Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kailima Ramadhani ameeleza kuwa kushiriki au kutoshiriki kwa vyama vya siasa kwenye uchaguzi sio habari mpya kwani ni suala ambalo limeshatokea kipindi cha nyuma.
“Kushiriki au kutokushiriki kwa Vyama vya Siasa sio habari mpya, miaka kadhaa vyama vingi havikuweza kushiriki, kwa mujibu wa sheria iwapo vyama vyote visiposhiriki basi hapo tume ingehairisha, akitokea mgombe mmoja anapita bila kupingwa,” – Kailima
Ameeleza kuwa kuna maeneo baadhi wa wagombea na watu wanaomba uchaguzi uahirishwe jambo ambalo haliwezekani kwani uchaguzi unaongozwa kwa mujibu wa sheria.
Zaidi amesema moja ya sababu za kisheria zinazoweza kufanya Tume ya Uchaguzi iahirishe uchaguzi wa eneo fulani ni kama kuna mgombea ambaye amepoteza maisha na si vinginenyo.
“Sitaki kuongea mengi, tumebana vyuma vilivyolegea” – JPM