December 21, 2017 imenifikia stori kutoka kwa Malkia, ambapo Naibu wa Waziri Mkuu wa nchini Uingereza, Damian Green, ameachishwa kazi kwa kukutwa na picha za ngono kwenye kompyuta yake ya ofisini na kushindwa kutoa taarifa zilizo sahihi kuhusu picha hizo.
Tofauti na kosa hilo Waziri huyo Damian Green alikuwa anachunguzwa pia juu ya madai ya kutowaheshimu wanawake wanaharakati ambao wako katika chama chake cha Conservative.
Inaelezwa kuwa Green amelazimishwa kuandika barua ya kuachia kiti chake cha Naibu Waziri Mkuu na Mkuu wake wa kazi Waziri Mkuu Theresa May baada ya kutokea tuhuma hizo.
Binadamu mzee zaidi duniani, mkoani Songwe amefariki dunia