Saa chache leo December 21, 2017 baada ya Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe kuonana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, Zitto amekutana pia na Mwenyekiti wa CHAUMMA Hashim Rungwe Spunda.
Ameeleza kuwa amekutana na Spunda ikiwa ni mwendelezo wa kukutana na viongozi wa juu wa vyama vya upinzani nchini.
Zitto amesema mazungumzo aliyofanya na Spunda ni sehemu ya maelekezo aliyopewa na Kamati Kuu ya ACT Wazalendo kuwafikia wadau wote wa Demokrasia nchini ili kuweka mikakati ya pamoja ya hatua za ziada za kuchukua ili kuboresha mazingira ya chaguzi huru na za haki nchini.
“Nafurahi tumekuwa na mazungumzo mazuri sana. Ndugu Rungwe ni mzee mwenye busara na hekima nyingi sana. Ni matarajio yetu kuwa mazungumzo haya yatazalisha jambo zuri kwa Taifa.” – Zitto Kabwe
“Tumeanza kuwatoa wapangaji wa ofisi na biashara, watu binafsi wajiandae” Shadrack Nkelebe