Mamlaka ya uvuvi na Bahari Kuu hivi karibuni imefanya ukaguzi katika Bandari ya Dar es Salaam ndani ya meli kutoka China ambayo imeomba kibali cha kuvua samaki aina ya Jodari katika ukanda wa Bahari ya Hindi.
Kwa mujibu wa Kaimu Afisa Udhibiti wa kusimamia Udhibiti Bahari Kuu, Daniel Kawiche nimemnukuu akisema, “watu kutoka nje wakiomba kibali kuvua ndani ya nchi kwa kawaida wanaomba leseni ya shughuli hiyo na masharti ya leseni hiyo ni pamoja na wao kuvua wakiwa pamoja na mabaharia 2 na mwangalizi wa Kitanzania”.
Ameeleza pia kuwa hii inasaidia katika kufanya uangalizi na kufuatilia kwa karibu shughuli zote za uvuvi zitakazofanyika ili kujua takwimu zote za kiasi cha samaki kilichovuliwa ili kuwepo na ukusanyaji sahihi wa mapato yanayotokana na shughuli hiyo pamoja na kuhakikisha hawajavua na kuchukua samaki wengine tofauti na walioombea leseni kuwavua.
Wema na Jokate wateuliwa na waziri wa maliasili