Ayo TV imefanya Exclusive interview na mchezaji mpira wa miguu maarufu wa Timu ya Taifa ya Wanawake Marekani Alexandra Morgan ambaye amekuja nchini kuhamasisha wanafunzi wa kike wanaopenda mpira wa miguu kucheza mpira wa miguu pamoja na michezo mingine wakiwa bado mashuleni ili kuwaongezea uwezo wa kufanya vizuri zaidi.
Ameeleza kuwa ameona wasichana wengi mashuleni wenye uwezo mkubwa wa kucheza soka lakini hawafahamu hatima yao pindi wanapomaliza masomo yao na kuongezea kuwa mashuleni wasichana hawapewi nafasi sana kwenye soka la wanawake na ndio maana amekutana na TFF ili kuwashauri mazuri ya soka hilo la wanawake.
“Elimu ni kipaumbele, na hata kwangu ilikuwa kipaumbele na ndio maana nilicheza mpira na kupata kipato kutokana na kucheza mpira kwasababu ya elimu niliyokuwa nimepata, na hii ni kutokana na nidhamu niliyoiweka kwenye elimu na kucheza soka, na ndio maana nataka kuelezea uzoefu wangu jinsi nilivyofanikiwa kwenye hili.” – Alexandra Morgan
Mambo matatu ya kufahamu kutoka Azam FC leo December