Watu 22 wanahofiwa kufa maji katika ajali iliyotokea katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma alfajiri ya kuamkia leo December 23, 2017 baada ya boti iitwayo Atakalo Mola kugongwa mtumbwi maarufu kama MV Pasaka.
Taarifa zinaeleza kuwa watu 115 walfanikiwa kuokolewa kwenye ajali hiyo huku miili ya watu wanne ikiwa imepatikana na imekwisha tambuliwa na ndugu zao.
Kwa mujibu wa Ofisa wa Sumatra Mkoa wa KigomaAmaniel Sekulu mtumbwi ulikuwa umebeba abiria 137 ambao walikuwa wanaelekea kwenye kungamano la kidini ikielekea kijiji cha Sunuka huku boti ikiwa imebeba abiria 65.
“Tunatafuta watafiti wenye uzoefu” -Naibu Waziri Mwanjelwa