Bara la Afrika ni miongoni mwa mabara yanayoongoza kwa umaskini duniani ukiachalia mbali nchi kama Nigeria, Angola na Afrika Kusini ambazo zinatajwa kuwa ni miongoni mwa nchi tajiri katika bara la Afrika kutokana na kuwa vizuri kiuchumi.
Leo December 23 2017 naomba nikusogezee TOP 5 ya nchi zinazotajwa Afrika kuongoza kwa umasikini.
5.Eritrea
Kwa mujibu wa tatafiti za GDP unaeleza kuwa Eritrea ambayo imewahi kutawaliwa na nchi za Italia 1869 na Uingereza 1941 wakati wa vita vita vya pili vya dunia, kwa mujibu wa GDP uchumi wa Eritrea upo chini kutokana na kuwa na uzalishaji mdogo wa asilimia 1.2 wa bidhaa zake.
4. Liberia
Liberia ni miongoni mwa nchi chache za Afrika ambazo hazijatawaliwa na nchi za Ulaya lakini inatajwa kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda mrefu nchini humo kabla ya amani kupatikana 2003 na uchaguzi wa demokrasia kukafanyika 2005, vita hivyo vimeifanya nchi hiyo kuwa duni kiuchumi na asilimia 85 ya raia wake wanaishi chini ya dola 1 kwa siku.
3. Burundi
Burundi ni miongoni mwa nchi za Afrika ambazo uchumi wake kwa kiwango kikubwa umeathiriwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na ukabila, Burundi 93% ya mapato yao inategemea uuzwaji wa kahawa nje ya nchi, 80% ya raia wake wanaishi katika umasikini na 57% ya watoto wana afya dhaifu sababu ya umasikini.
2. Zimbabwe
Zimbabwe haijaishia kutajwa kama nchi masikini tu duniani lakini pia inatajwa kama ni nchi ambayo watu wake wanafariki wakiwa na umri wa miaka 37 kwa wanaume na wanawake 34 hii inatokana na asilimia 20.1 ya watu wa Zimbabwe kuishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
1- Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
Hadi kufikia miaka 1997 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilikuwa ikijulikana kama Zaire, ilianza kutajwa kama nchi masikini duniani mapema kwenye mwaka 2010, nchi hiyo uchumi wake umeathiriwa na vita vya pili vya Congo vilivyoanza 1998, Congo inatajwa kuwa ndio nchi kubwa duniani inayoongoza raia wake kuzungumza lugha ya kifaransa ikiwa na watu zaidi ya milioni 71 ikiizidi Ufaransa kwa tofauti ya watu milioni 6.
SOURCE: africanranking.com
“Tumeanza kuwatoa wapangaji wa ofisi na biashara, watu binafsi wajiandae” Shadrack Nkelebe