Mwanasheria mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambae yuko katika mataibabu Nairobi ameweza kusimama kwa mara ya kwanza baada ya kushambuliwa.
Tundu Lissu amekuwa akipokea matibabu Nairobi tangu alipopigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma mwezi September, 2017.
Katika picha iliowekwa katika ukurasa wa Facebook wa CHADEMA, Mbunge huyo anaonekena akisimama akisaidiwa na wahudumu wawili wa hospitali.
Ujumbe ulioambatana na picha umesema “Wiki iliyopita niliwataarifu kwamba madaktari wangu wamesema ‘nitasimama, nitatembea na nitarudi Tanzania. Leo Boxing Day (Tarehe 26 Disemba) nimeweza kusimama kwa mguu mmoja. Hatua inayofuata ni magongo kesho na nitawajulisheni hatua nyingine katika matibabu yangu.”
“TUWAULIZE TSH MILIONI 360 WALIMPA NANI?” – MOLEL, BONYEZA PLAY KUMTAZAMA