Leo December 27, 2017 zimevuma taarifa katika mitandao ya kijamii kumhusu Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya kwamba ana mpango kuhama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili ajiunge na Chama cha Mapinduzi (CCM)
Mboya ameongea na AyoTv na millardayo.com na kukanusha taarifa zilizosambazwa kwamba anampango wakuhama CHADEMA na kuongeza kuwa yeye ameingia kwenye Siasa kwa malengo na kwa ajili ya kuwatumikia wananchi hadi malengo yake yatakapotimia.
“Si kila mtu aliyeingia kwenye siasa ameingia kwa njaa, wengine tumeingia kwa malengo, nikitoka huku niseme nilifanya hivi na hivi, nitamuunga mkono Rais kwa kufanya kazi na mimi, niwaambie tu wakazi wa Moshi wapuuze,” – Meya Mboya
“USIPELEKE SHIDA ZAKO MWAKA UNAOKUJA” – ASKOFU KILAINI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA