Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi nchini Zimbabwe Constantin Chiwenga ambae ndiye aliongoza jeshi kumuondoa madarakani Robert Mugabe, ameteuliwa kuwa Makamu mpya wa Rais wa Zimbabwe akichukua nafasi aliyokuwa anaishikilia Rais wa sasa wa taifa hilo Emmerson Mnangagwa.
Amestaafu nafasi ya ukuu wa jeshi December 23, 2017 na kuwa Naibu wa chama tawala cha Zanu-Pf
Rais mpya Emmerson Mnangagwa alichukua mamlaka baada ya jeshi kuingilia kati tarehe 15 mwezi November kufuatia mgogoro wa kumrithi Robert Mugabe uliozuka kati Mke wa Mugabe na Emmerson Mnangagwa ambaye alikuwa Naibu Rais wa Zimbabwe.
HUYU NDIO GEORGE WEAH KUTOKA USHINDI WA BALLON D’OR HADI URAIS, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA