Leo December 28, 2017 President John Pombe Magufuli amefika katika ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma zilizopo Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam ambapo amewasilisha fomu yake ya tamko kuhusu rasilimali na madeni katika ofisi hiyo.
JPM ameipongeza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kazi inazofanya na amemtaka Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Harold Nsekela kutopokea fomu ya kiongozi yeyote ambaye atakuwa hajawasilisha tamko lake ifikapo tarehe December 31, 2017.
Namnukuu alichoagiza JPM, “Jaji Nsekela ikifika December 31, ambayo ni siku ya mwisho kwa Mujibu wa Sheria, weka mstari na usipokee fomu zingine, halafu tuone sheria itafanyaje, nakutakia kazi njema” – President JPM
Baada ya maneno hayo ya JPM, Jaji Mstaafu Harold Nsekela amemshukuru na kumpongeza Rais Magufuli kwa kutekeleza matakwa ya kisheria yanayomlazimu kujaza fomu hizo na amesisitiza kuwa ujazaji wa fomu hizo kwa viongozi wa umma sio ombi.
“Viongozi hawaombwi kujaza fomu hizi, kuna baadhi wanadhani labda kutuletea hilo tamko ni fadhila, hapana, sheria ya nchi inahitaji hivyo na kuna sababu zake za msingi,” – Jaji Nsekela
Jaji Mstaafu Nsekela amempongeza President Magufuli kwa kuwasilisha taarifa ya akaunti yake ya benki na amekiri kuwa ameonesha mfano wa kuigwa na viongozi wengine.
KIKUNDI CHA VIJANA WAZALENDO KIMEZUNGUMZA KUHUSU ALIYOFANYA JPM 2017, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA