Zikiwa zimepita saa 19 toka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli awasilishe fomu zake za tamko la Rasilimali na madeni katika Ofisi ya Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe naye ameonyesha fomu hizo ambazo zinaonyesha mali,mshahara na madeni anayodaiwa.
Fomu alizoonyesha Zitto Kabwe ni za mwaka 2016 kama sheria inavyoagiza, ambapo kwenye ukurasa wa mwisho ameandika baadhi ya taarifa mpya ikiwemo kufunga ndoa ambapo katika taarifa zake za awali hakua ameoa, mali ambazo ameandika ni pamoja na ardhi anayomiliki kwa asilimia 50 ya plot 34 Mkoani Mtwara yenye ukubwa wa Square meter 33,019.
Uliiona hii ya Zitto Kabwe alivyofunguka kuhusu Takwimu za pato la Taifa?Bonyeza play kutazama.