Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr. Mwigulu Nchemba amewaagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mtwara kushirikiana kwa pamoja katika zoezi la uandikishaji wa kitambulisho cha uraia ili pasiwepo na ambao si Raia wa Tanzania kuandikishwa.
Waziri Dr. Nchemba amewataka Watanzania hasa maeneo ya mipakani kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha kwa ajili ya vitambulisho vya uraia na kuwafichua wale ambao si Raia wa Tanzania ambao wamejitokeza sasa kuandikishwa ili pasiwepo baadae kesi za wasio Watanzania kupata uraia.
M/KITI UVCCM- “UKILEWA MADARAKA UNAJIANDALIA MAZINGIRA MABAYA BAADA YA MADARAKA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA