Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza amekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Tamasha la Tanzania Tukuza Utalii Festival kwa ajili ya kukuza utalii lililoandaliwa na Shirikisho la Waimbaji wa Nyimbo za Injili chini ya Mkurugenzi Godwin Maimu.
Akiongea katika Tamasha hilo Juliana Shonza amewataka wasanii kutii agizo alilolitoa President Magufuli la kuwataka kuvaa nguo zenye staha katika video na wanapokuwa jukwaani.
“Wasanii wote ambao wataendelea kukaidi agizo la kuvaa mavazi ya staha, Wizara yangu haitawavumilia, tutachukua hatua kwa yoyote bila kujali nafasi au umaarufu wake, kabla dhoruba haijawakumba wabadilike, kwenye kupiga rungu siangalii mtu usoni,”– Juliana Shonza
MAGAZETI LIVE: AKAUNTI YA JPM BENKI ILIVYOSHTUA VIGOGO, LISSU AANZA VITA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA