Rais aliyeondolewa madarakani leo December 30, 2017 amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa tuhuma za kuvivunjia heshima vyombo vya mahakama.
Muhammad Mursi aliyekuwa Rais wa Misri amehukumiwa hukumu hiyo leo ikiwa bado anaendelea kuzuiliwa katika jela za nchi hiyo huku akiwa tayari amekwisha hukumiwa mara kadhaa ikiwemo kifungo cha maisha.
Mbali na Muhammad Mursi, mahakama ya Misri pia imewahukumu watu 18 wengine kwa tuhuma hiyohiyo ya kuivunjia heshima mahakama. Aidha mahakama ya Misri imemtaka Mursi kulipa faini ya Pauni milioni moja za Misri kwa jaji Muhammad al-Nemr.
UJUMBE WA ASKARI MWANZA MUDA MCHACHE KABLA YA KUJINYONGA(audio), BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA