Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, ameuzungumzia mwaka 2017 huku akiukaribisha mwaka mpya 2018, kwa kusema kuwa tukio la kupigwa risasi Tundu Lissu lilimgharimu.
Katika ukurasa wake wa facebook Zitto Kabwe amesema kupigwa risasi kwa Tundu Lissu ni tukio lililomfanya kubadili mtazamo wake na kumfanya kupoteza watu wa karibu.
“Tukio la kupigwa risasi Mbunge Tundu Lissu ni tukio baya sana na lilibadilisha kabisa mtazamo wangu wa mapambano ya kulinda Demokrasia. Ilinigharimu kwa kupoteza watu wa karibu kufuatia kuwa mkali sana kulaani tukio lile.” – Zitto Kabwe
“Sijutii kwani niliamini kuwa lengo la waliotaka kumwua Lissu lilikuwa kutunyamazisha na hivyo majibu sahihi yakawa ni kusema zaidi,” – Zitto Kabwe.
Zitto Kabwe ameendelea kwa kusema kuwa tukio lingine alilokumbana nalo 2017 ni kitendo cha kuondoka kwa wanachama waandamizi na kuhamia chama kingine, huku akilielezea kuwa limekuwa funzo kubwa kwake.
“Kuondoka wanachama waandamizi ilikuwa pigo. Pigo hili limetupa funzo kubwa Sana na hivyo Tutaendelea kuwepo na imara zaidi mwaka 2018,” – Zitto Kabwe.
BREAKING: MBOWE AZUNGUMZA NA WAANDISHA KUHUSU KAKOBE, SERIKALI NA MENGINE