Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa leo January 1, 2018 ameshiriki ibada ya Mwaka Mpya katika kanisa la KKKT Usharika wa Monduli ambapo amewaomba Watanzania wakatae kugawanywa kwa sababu yoyote ile, kwani umoja ni mshikamo.
“Tunapouanza mwaka huu mpya niwaombe watanzania wenzangu tukatae kugawanywa kwa sababu yoyote ile.Umoja na mshikamano ndio nguzo yetu,” – Lowassa
Pia Lowassa amesema anazishukuru taasisi zote za kidini kwa mchango wao katika amani ya nchi.
“Taasisi hizi za kidini zimekuwa mstari wa mbele siku zote katika kuendeleza sekta za afya, elimu, maji na nyingine nyingi. Wanastahili pongezi nyingi,” – Lowassa.
UJUMBE WA ASKARI MWANZA MUDA MCHACHE KABLA YA KUJINYONGA (audio)