Leo January 1, 2018 Ofisi ya Makamu wa Rais imetoa taarifa ya kusikitisha baada ya kutokea kwa kifo cha Mke wa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.
Katika taarifa hiyo ya masikitiko, Ofisi ya Makamu wa Rais imebainisha kuwa mke Naibu Waziri wa Nchi, Kangi Lugola ambaye ni Mary Lugola amefariki dunia majira ya asubuhi ya leo jijini Dar es Salaam.
Pia taarifa hiyo imemalizia kwa kusema “Taarifa zaidi taratibu za mazishi zitatolewa baadaye, Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi,”