Leo January 1, 2018 hali ya sintofahamu imetawala baada ya mchora katuni maarufu, Masoud Kipanya kudaiwa kukamatwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kuchora katuni inayosemekana ni ya uchochezi.
Hata hivyo, Uongozi wa Clouds Media umewaomba Watanzania kuendelea kuwa katika hali ya utulivu wakati ikiendelea kuzifanyia kazi taarifa kamili wapi alipo Masoud Kipanya, ambapo baadaye uongozi utatoa taarifa za kina.
#TaarifaKwaUmma
•Uongozi wa Clouds Media Group (CMG) unawaomba wananchi wote nafasi ya utulivu wakati tukiendelea kuzifanyia kazi taarifa kamili wapi alipo @masoudkipanya. Uongozi utaoa majibu ya kina.
— Clouds Media (@CloudsMediaLive) January 1, 2018
KITU PAPII KOCHA KAMFANYIA RAIS JPM, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA