Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, Mohamed Mpinga ameongea na mwandishi wa AyoTv na millardayo.com na kuelezea sababu zilizofanya wao kumkamata Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi wa CHADEMA maarufu kama ‘Sugu’.
Kamanda Mpinga amesema wamemkata Sugu pamoja na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga kutokana na kauli walizotoa katika mkutano wa hadhara uliofanyika tarehe 30,December 2017 mkutano ambao uliitishwa na Mbunge huyo.
“Ni kweli tumemkamata kwa ajili ya mahojiano yeye pamoja na Katibu wa Kanda wa CHADEMA, kutokana na kile walichosema, walitoa matamko ambayo yangeweza kusababisha wananchi kuichukia serikali au serikali kuwachukia wananchi wao,” -Kamanda Mpinga
ALICHOONGEA RAIS MAGUFULI KWA BABU SEYA NA WATOTO WAKE IKULU LEO