Leo January 3, 2018 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Dr. Mary Mwanjelwa amezungumza na wananchi na mafundi wanaojenga majengo ya Shule ya Sekondari Iyera iliyopo mkoani Mbeya ili kutatua changamoto ya vyumba vya madarasa kwa ajili ya kuhimili wingi wa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza.
Dr.Mwanjelwa amesema “tangu serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na President Magufuli kutangaza utoaji elimu bure kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi sekondari kumekuwa na ongezeko kubwa la wananfunzi wanaojiunga na masomo.”
Mwanjelwa amesifu juhudi za Uongozi wa Wilaya ya Mbeya kwa kushirikiana kwa pamoja na wananchi katika shughuli za maendeleo huku akiipongeza Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa kufanya vyema kwa kuongoza kwa ufaulu wa wanafunzi dhidi ya Halmashauri zingine za Mkoa wa Mbeya.
Dr. Mary Mwanjelwa ameongeza nguvu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule hiyo ya Sekondari Iyera kwa kuchangia mifuko 20 ya saruji.
LIVE: BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU WANAZUNGUMZA NA WAANDISHI.