Leo January 3, 2018 Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imezungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa kiasi cha Tshs Bilioni 285 bado ni madeni ya wadaiwa sugu wa mikopo ya elimu ya juu tangu mikopo ianze kutolewa kwa wanafunzi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul Razaq Badru, bodi itaendelea kukagua taarifa za mishahara za waajiri wote waliosajiliwa na kuwataka kuwakata wanufaika marejesho ya mikopo waliyopata wakiwa chuo, lengo likiwa kufikia kukusanya Tsh Bilioni 17 ifikapo Mwezi July, 2018 tofauti kiwango kinachokusanywa sasa cha Tsh Bilioni 13.
Ameongoza kuwa tangu mwaka jana bodi hiyo imeweza kuwapata wadaiwa sugu wa mikopo hiyo 26000 ambao wako kazini.
Jeshi la Polisi Arusha limefanya ukaguzi wa magari na kukutana na makosa haya
“Mimi mporipori nimekuwa mwenyekiti, vijana biskuti hawana nafasi” -Mwenyekiti UVCCM