Leo January 3 , 2018 Upande wa utetezi umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wanapata tabu wakiambiwa upelelezi wa kesi inayomkabili Mhasibu Mkuu wa (TAKUKURU), Godfrey Gugai anayedaiwa kumiliki mali zenye thamani ya Tshs Bilioni 3 ambazo haziendani na kipato chake kuwa haujakamilika.
Hayo yameelezwa na Wakili wa Utetezi, Semi Malimi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya wakili wa serikali, Peter Vitalis kueleza upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.
Wakili Malimi amedai kuwa shauri hilo lilianzia kama la kinidhamu wakati Gugai akiwa kazini, hivyo wanapata shida wakiambiwa upelelezi wake haujakamilka.
Hata hivyo, wakili Vitalis amedai kuwa shauri lililopo mahakamani ni la jinai na sio la kinidhamu kama ilivyoelezwa na kwamba lina makosa ya utakatishaji fedha, hivyo uchunguzi wake unahusisha taasisi zaidi ya moja.
Baaada ya kueleza hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi January 15, 2018.
MAHAKAMANI: Walichosema TAKUKURU kuhusu nyaraka walizoomba kutoka kwa Aveva
Muhasibu “BILIONEA” wa TAKUKURU kajisalimisha