Nchi ya Iceland imekuwa nchi ya kwanza duniani kuharamisha wanaume kulipwa zaidi ya wanawake ambao wanafanya kazi moja.
Sheria hii mpya imepitishwa January 1, 2018 japokuwa ilikuwa imeanza kufanyiwa kazi ili kuhalalishwa tangu Siku ya Wanawake Duniani March 8, 2017.
Kupitia sheria hii mpya, makampuni, mashirika na taasisi za kiserikali zilizo na wafanyakazi zaidi ya 25 zitalazimika kupata kibali maalumu cha serikali kwa ajili ya utekelezaji wa sera hizo za malipo sawa kati ya wanawake na wanaume.
Inaelezwa kuwa waajiri watakaokiuka sheria hii mpya, hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. Hatua hii inalenga kuleta usawa katika maeneo ya kazi bila kujali jinsia. Nchi za Scandnavia ambazo ni pamoja na Denmark, Finland, Iceland, Norway na Sweden zimeahidi kuwa zimetokomeza na kuziba pengo la malipo ya mishahara baina ya wanaume na wanawake ifikapo mwaka 2022.
Watu watatu wahukumiwa kifungo cha maisha jela mkoani Kagera
Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu imezungumza kuhusu wadaiwa sugu wa mikopo