Leo January 4, 2018 President John Pombe Magufuli amepokea barua kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni iliyowasilishwa ikulu na Mjumbe Maalum Sam Kutesa ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda.
Baada ya kupokea barua hiyo President JPM amefanya mazungumzo na Waziri huyo Sam Kutesa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Kutesa amesema Rais Museveni amemtumia President Magufuli na Watanzania wote kwa ujumla salamu za heri ya mwaka mpya na pia wamezungumza kuhusu uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda.
Kutesa amezungumzia jinsi Uganda inavyofurahishwa na kuridhishwa na uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati Uganda na Tanzania, mazungumzo yao ya leo yamejikita kuimarisha uhusiano zaidi kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili.
Namnukuu Sam Kutesa “Tumezungumza namna tutakavyoimarisha na kukuza zaidi uhusiano wetu katika maeneo mbalimbali, kama unavyojua kuna miradi ya maendeleo ya ushirikiano ukiwemo mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Bandari ya Tanga,Tanzania na miradi mingine na masuala.”
ALICHOONGEA RAIS MAGUFULI KWA BABU SEYA NA WATOTO WAKE IKULU LEO, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA