Leo January 4, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu miaka 30 jela watu watano akiwemo Mfanyabiashara Moriss Malianga maarufu kama ‘Rais wa Sinza’ baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la unya’nganyi wa kutumia silaha.
Wengine waliohukumiwa ni pamoja na Flano Masulu (Singu), Jeremiah Mgori, Sandru Kamugisha na Sadick Bwanga. Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambapo amesema mahakama imeridhika na ushahidi wa upande wa mashtaka ambao umethibitisha mashtaka dhidi yao.
Awali katika kesi hiyo namba 14 ya mwaka 2016, wakili wa utetezi Nehemiah Nkoko aliomba wateja wake wapatiwe nafuu ya adhabu. Katika kesi hiyo, washtakiwa wanadaiwa December 22, 2015 maeneo ya Mabibo Luhanga washtakiwa waliiba Dola za Marekani 8,600 ambayo ni sawa na Sh.Mil 18 kwa wakati huo.
Pia wanadaiwa waliiba tena Tsh milioni 2.5, laptop moja na simu nne vyote vikiwa ni mali za Anderson Balongo na baada ya kuiba walimtishia kwa bastola Zeno Mriwa, Aneth Paulo, John Mkundi ili kujipatia mali hizo.
MAHAKAMANI: Walichosema TAKUKURU kuhusu nyaraka walizoomba kutoka kwa Aveva
Muhasibu “Bilionea” wa TAKUKURU alivyofikishwa Mahakamani