Stori kuhusiana na ishu za Mikopo ya Elimu ya Juu zinaendelea kuchukua headlines nchini baada ya juzi Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi HESLB, Abdul Razaq Badru alitangaza kuwapata baadhi ya wadaiwa sugu na kuwakata fedha kwa ajili ya malipo ya mikopo yao.
Jana January 3, 2018 katika moja ya Gazeti nchini ilichapishwa taarifa ya Mwl. Ndyamukama akimuomba Waziri Mkuu amsaidie arejeshewe fedha alizokatwa kimakosa na Bodi ya Mikopo.
Leo January 4, 2018 Dr. Hassan Abbas kupitia ukurasa wa Twitter wa Msemaji wa Serikali ametoa taarifa juu walipofikia kuhusu suala hilo.
“Tumefuatilia malalamiko hayo na suala hilo limepatiwa ufumbuzi. Atarejeshewa fedha zake Jumanne ijayo.” – Dr Hassan Abbas
TAARIFA: Gazeti la UHURU la jana ukurasa wa 15 kuna barua ya Mwl. Ndyamukama akimuomba Waziri Mkuu amsaidie arejeshewe fedha alizokatwa kimakosa na Bodi ya Mikopo.
Tumefuatilia malalamiko hayo na suala hilo limepatiwa ufumbuzi. Atarejeshewa fedha zake Jumanne ijayo.
Dkt. H.A.
— Msemaji wa Serikali (@TZ_MsemajiMkuu) January 4, 2018
VIDEO: BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU IMEZUNGUMZA KUHUSU WADAIWA SUGU WA MIKOPO
MEYA JACOB AFUNGUKA BAADA YA KUDAIWA KUPIGANA KATIKA UCHAGUZI DSM