Leo January 4, 2018 Wajumbe wa Chama cha Wamiliki wa mabasi nchini TABOA wamelazimika kutoka katika mkutano ulioitishwa na Mamlaka ya Uthibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini-SUMATRA- na kuacha mkutano huo ukiendelea.
Hii ni baada ya kuzuiwa kutoa tamko dhidi ya kanuni mpya za usafiri wa barabarani zinazotarajiwa kuanza kazi January 15 mwaka huu.
katika mkutano huo kabla ya maombi ya kutoa tamko hilo, baadhi ya wanachama cha TABOA wamehoji vigezo vilivyotumika kuongeza faini ya makosa ya barabara hadi kufikia kati ya shilingi laki mbili na nusu na laki tano huku wengine wakihoji kosa la mwendokasi kumhusu mmiliki badala ya dereva anayeendesha gari husika.
Akizungumza katika mafunzo hayo Meneja wa Leseni Mkoa wa Arusha Deo Ngowi amesema lengo la kuwakutanisha wadau wa usafiri ni kupitia upya rasimu ya sheria mpya za usafirishaji na kuzijadili na kuzipitisha ili zitumike kama kanuni mpya za usafirishaji.
‘Rais wa Sinza’ na wenzake watano wahukumiwa jela miaka 30
Barua aliyoipokea leo JPM toka kwa Rais Museveni