Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye yuko kwenye matibabu Nairobi Nchini Kenya baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana September 7, 2017 baada ya kumaliza vikao vya Bunge akiwa nje ya nyumba yake, leo January 5, 2018 amezungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza nchini humo.
Lissu amewashukuru Madaktari na wauguzi waliojitahidi kwa kadri wawezavyo kuokoa maisha yake na kueleza kuwa hali yake inaendelea kuimarika kila siku.
Vilevile amewashukuru watu wote hususani Watanzania ambao walitoa michango mbalimbali ili kufanikisha gharama zake za matibabu.
Lissu amesema alipigwa risasi 16, nane zilitolewa hospitalini Dodoma kabla hajapelekwa Nairobi, saba zikitolewa hospitalini Nairobi na moja bado iko mwilini.
Amesema kwa mujibu wa madaktari risasi hiyo iliyo mwilini mwake kuitoa itakuwa hatari zaidi kwa maisha yake kuliko kuiacha.
“Risasai zilizoingia katika sehemu mbalimbali za mwili wangu ni 16, zilizobaki ndani ya mwili zilikuwa 8 Madaktari wa Dodoma pamoja na hapa Nairobi walitoa risasi 7, risasi moja bado haijatolewa Madaktari wamesema mahali ilipo haina madahara itakuwa na madhara zaidi wakijaribu kuitoa,” – Tundu Lissu
MSIBA: MWANAMUZIKI MKONGWE WA DANSI AFARIKI DUNIA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA
FULLVIDEO: BABU SEYA NA PAPII KOCHA RASMI WAINGIA STUDIO, WAZUNGUMZA HAYA