January 8 2010 ni siku ambayo taifa la Togo haliwezi kuisahau siku hiyo kutokana na shambulio kubwa liliwatokea wachezaji wao wa timu ya taifa ya Togo wakiwa Angola katika mji wa Cabinda kwa ajili ya michuano ya AFCON.
Tukio hilo ambalo liligharimu maisha ya watu wawili waliyokuwemo kwenye basi la timu na kujeruhi watu wengine, alikuwepo pia nahodha wa timu ya taifa ya Togo anayecheza club ya İstanbul Başakşehir ya Uturuki Emmanuel Adebayor pamoja na staa wa zamani wa Yanga aliyekuwa anaichezwea timu ya taifa ya Togo Vincent Bossou.
Adebayor hawezi kusahau tukio hilo na leo January 8 2018 linatimiza miaka nane toka washambuliwe, kupitia ukurasa wake wa instagram Adebayor ameandika hivi.
“January 8 2010 – January 8 2018 ni miaka nane toka basi la wachezaji wa Togo lishambuliwe na magaidi tukiwa Cabinda, bado nasikia kelele za majonzi, machozi na milio ya risasi, miaka imeenda lakini maumivu bado yamebaki watu wawili waliuwawa na wengine kujeruhiwa siku hiyo, naziombea familia zote na wachezaji waliyokuwemo katika shambulio hilo Asante kwa kila kitu wacha tubaki imara na tushikamane”>>>Adebayor
Bossou wa Yanga kataja mchezaji wa Tanzania anayeamini anaweza kucheza Ulaya