Kitengo cha Uhamiaji kimewaondoa watu waliotuma maombi ya kazi wakati wa zoezi la kukusanya wafanyakazi wapya kwa sababu ya kubadilisha rangi ya miili yao maarufu kama kujichubua na wenye michirizi mwilini nchini Ghana.
Msemaji wa kitengo cha Uhamiaji amesema kuwa wamewaondoa kwa sababu wanaweza kupata majeraha na kutokwa na damu wakati wakiwa kwenye mafunzo.
Baadhi ya raia Waghana wamepinga hatua hiyo na kusema ni ubaguzi, huku baadhi wakikasirishwa zaidi na waliondolewa kwa vigezo cha kuwa na michirizi mwilini.
Baadhi watu wamesifia hatua ya kuwaondoa waliobadili rangi zao za mwili. Walioondolewa wengine ni wenye michoro mwilini (tattoo) na wenye rasta.
Waliotuma maombi ya ajira wanapitia vipimo vya mwili na afya kama sehemu ya zoezi la kuwachuja wenye vigezo. Watu 84,000 walituma maombi ya kazi hiyo, huku wanaohitajika wakiwa ni 500 pekee.
VIDEO: GIGY MONEY ATOKWA MACHOZI NJE YA OFISI ZA BASATA “HAKUNA FREEDOM”
VIDEO: BAADA YA KUFUNGIWA KUIMBA NA KUPOST MITANDAONI KWA MIEZI 6, PRETTY KIND AMEYASEMA HAYA