Leo January 10, 2017 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Watoto, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ametembelea Hospitali ya Taaluma ya Tiba ya Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila ambako ametoa maagizo kadhaa.
Waziri Ummy ameagiza kuwa Idara nzima ya magonjwa ya ndani ya Hospitali ya Muhimbili kuhamia mara moja katika hospitali hiyo ya Mloganzila ikiwa ni pamoja na madaktari, madaktari bingwa, wauguzi na wataalamu wengine kwenye idara hiyo.
Pia ameagiza wagonjwa walio kwenye wodi namba 3, 4, 5, 6, 7 na 8 za jengo la Mwaisela hospitalini Muhimbili pia wahamishiwe Mloganzila isipokuwa wale walio mahututi ili kwamba wodi hizo zifanyiwe ukarabati.
“Nawaagiza waganga wafawidhi wa hospitali za rufaa za Temeke, Mwananyamala na Amana kuanzia sasa rufaa zote za wagonjwa wa magonjwa ya ndani zije Mloganzila.” – Waziri Ummy Mwalimu
“Asilimia 12 ya vifo vyote nchini hutokana na saratani ya matiti” – Wizara ya Afya
Mpango wa huduma ya afya bure kwa Wazee uliozinduliwa na Waziri wa Afya