Leo January 10, 2018Mtu wangu wa nguvu nakusogezea miji kumi Afrika inayoongoza kwa usafi, good news ni kwamba Tanzania upo mji mmoja ambao umetajwa katika list hii .
Ifahamu miji 10 Afrika inayoongoza kwa usafi
10.Windhoek(Namibia)
Windhoek ni mji mkuu na mkubwa katika taifa la Namibia ambapo wameeneza njia za ubunifu katika utunzaji wa mazingira katika mji huo ambazo zinazosaidia kuhifadhi na kutunza mazingira, kitendo ambacho kimesaidia mji huo kuwa nafasi ya kumi kwa usafi.
9.Dar Es Salaam(Tanzania)
Dar es Salaam ni mji mkubwa na ndio kitovu cha uchumi Tanzania pamoja na umuhimu wake huo mkubwa kitaifa uliwahi kutajwa kuwa miongoni mwa miji michafu Afrika lakini kwa sasa mambo ni tofauti na Dar es Salaam inatajwa kama moja kati ya miji misafi Afrika.
8.Libreville(Gabon)
Pamoja na Libreville kuwa ni mji Mkuu wa Gabon na kuwa ndio mji Mkubwa katika taifa la Gabon, pia umetajwa katika list ya miji 10 misafi katika bara la Afrika na muonekano wake ni kama baadhi ya miji ya ulaya kutokana na utengenezaji wao wa barabara.
7.Accra (Ghana)
Accra ni mji Mkuu wa Ghana na ulikuwa ni kitovu cha Waingereza wakati wa utawala wao katika nchi hiyo na inajitahidi katika kutunza mazingira na ipo katika nafasi ya saba.
6.Tunis(Tunisia)
Tunis ni mji mkuu wa Tunisia unatajwa katika nafasi ya sita katika miji kumi Afrika inayoongoza kwa usafi. Manispaa ya mji ndio inahusisha kuuweka mji huo kuwa safi ukilinganisha na miji mingine ya Afrika kaskazini.
5.Gaborone(Botswana)
Gaborone pamoja na kuwa ni mji Mkuu wa Botswana lakini unatajwa kama ndio mji mkubwa kwa taifa la Botswana na miongoni mwa miji inayokuwa kwa kasi duniani ukuaji wa mji huo kwa haraka umesaidia mamlaka husika kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo usafi.
4.Nairobi(Kenya)
Mji wa Nairobi upo katika nafasi ya pili Afrika Mashariki kutajwa Katika list hii baada ya Dar es Salaam, Nairobi pia unatajwa kama mji unaovutia kwa kuwa na uoto wa kijani, July 2014 Gavana wa Nairobi alitoa magari 14 ya kukusanya uchafu kitendo ambacho kimesaidia mji huo kuthibiti uchafu.
3.Johannesburg(South Africa)
Johannesburg upo nafasi ya tatu katika miji 10 misafi Afrika lakini pia unatajwa katika list ya miji 50 duniani iliyokuwa imekamilika kwa ukuaji wa kimanedeleo maeneo ya mijini, ni mji wa Afrika ambao una majengo marefu, garden, parks na makazi ya watu, mamlaka za jiji hilo limewahamasisha watu kujitolea kutunza mazingira kitu ambacho kimesaidia mji huo kuwa msafi.
2.Port Louis(Mauritius)
Port Louis ni mji ambao unaongoza kwa umaarufu zaidi katika nchi ya Mauritius lakini pia ni mji unaotegemewa katika uchumi wa Mauritius, kuwepo kwa majengo na nyumba nzuri kumesaidia Manispaa ya mji huo kuusimamia mji katika usafi.
1.Capetown(South Africa)
Cape Town unatajwa kama ni miongoni mwa miji yenye mvuto na umewahi kushinda tuzo mbalimbali za kimataifa kutokana na mvuto wake na kutembelewa na watalii wengi, mamlaka husika pamoja na wakazi wa mji huo wamefanikiwa kuutunza mji huo na kuufanya kuwa safi.