Baada ya kamati ya nidhamu ya TFF kukaa na kupitia kesi kadhaa, wengi walitaka kufahamu maamuzi ya kamati ya nidhamu ni yapi kwa staa wa Yanga raia wa Zambia Obrey Chirwa ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa makosa kadhaa ya utovu wa nidhamu.
Baada ya afisa mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Boniface Wambura kukutana na waandishi wa habari leo alilazimika kujibu vipi yaliojiri kwenye kikao cha kamati ya nidhamu, vipi Chirwa amefungiwa au kasimamishwa?
“Kwenye suala la Chirwa hatujamfungia tumemsimamisha kwa tuhuma za utovu wa nidhamu na tumempeleka kwenye kamati ya nidhamu, wiki iliyopita ilikaa na kusikiliza kesi tano kati ya saba ambazo ikiwemo na Chirwa na afisa habari wa Toto ambao wataitwa wiki hii”>>>Wambura
Baada ya kipigo “Shida yangu mimi ni msemaji na shabiki wa hii timu”-Manara