Hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi 2018 imeendelea tena leo Jumatano ya January 10 2018 kwa michezo miwili kuchezwa huku mchezo wa kwanza ukiwa ni mchezo kati ya Yanga dhidi ya URA na mchezo wa baadae utakuwa ni Singida United dhidi ya Azam FC.
Game ya Yanga dhidi ya URA ya Uganda ililichezwa katika uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar lakini hadi dakika 90 za mchezo huo zinamalizika, matokeo ya game yalikuwa 0-0 ndipo mikwaju ya penati ilipolazimika kutumika ili kumpata mshindi.
URA ambao ni Mabingwa wa michuano hiyo wa mwaka juzi wamefanikiwa kuiondoa Yanga katika michuano hiyo kwa kuifunga kwa mikwaju ya penati 5-4, huku Obrey Chirwa ambaye hakuwepo katika kikosi kwa muda amekosa penati na mtandaoni kuanza utani kuwa Chirwa ameikatia Yanga tiketi za boti kurejea Dar es Salaam baada ya kukosa penati.
Obrey Chirwa wa Yanga amefungiwa?